NA MADINA ISSA
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA) Zanzibar imedhamiria kufanya mabadiliko ya kiufundishaji pamoja na kuimarisha mitaala ya elimu ili kupatikana kwa matokeo bora kwa wanafunzi.
Akizungumza katika ufungaji wa kambi ya mafunzo ya walimu wa skuli mbali mbali, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ali Khamis Juma, alisema mabadiliko hayo ni pamoja na kupunguza idadi ya masomo katika ngazi za msingi na sekondari na kuwa kati ya masomo saba hadi nane.
Alisema kufuatia mabadiliko hayo ni vyema walimu kuwa tayari kuyafanyia kazi mabadiliko kwa kufundisha kulingana na mazingira yatakayompa wepesi mwanafunzi kufahamu ili lengo la serikali la utoaji wa elimu bora liweze kufikiwa.
Alisema kuwa walimu wana kazi ngumu katika ufundishaji lakini kupitia mafunzo hayo wanatakiwa kujiamini na kuwa wabunifu hasa kwa wanafunzi wenye uwezo mdogo wa ufahamu ili kuepusha kufanya vibaya kwa wanafunzi hao.
Hivyo, aliwataka kuwa tayari katika kuyafanyia kazi mafunzo kwa vitendo kwani Taifa linawategemea na kuwakumbusha kuwa wajibu wao wajibu wao kuongeza bidii katika kuleta mabadiliko ili kukuza viwango vya elimu na kuongeza idadi ya ufaulu
Mkuu wa miradi ya taasisi ya Milele Zanzibar foundation, Khadija Ahmed Sharif, alisema milele imelenga kuharakisha shughuli za kimaendeleo katika mambo mbali mbali ikiwemo ya kielimu ili kusaidia kuleta mabadiliko katika sekta hiyo haswa katika maswala ya ufundishaji.
Hivyo, aliwataka walimu kuwasaidia walimu wenzao ili kuweza kuwapa uelewa walimu wote.
Nao walimu waliopatiwa mafunzo hayo, wamesema mafunzo hayo yataleta mabadiliko makubwa katika skuli zao hivyo, waliomba taasisi ya Milele kuendelea kushirikiana ili kuongeza