KIGALI, RWANDA
MAOFISA wa Afya Rwanda wamesema kuwa wakati wagonjwa 750 wanapatikana kila mwaka na saratani ya shingo ya kizazi, wengi huachwa bila kugundulika kwa sababu ya ukosefu wa uelewa.
Hayo yalielezwa wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa saratani ya kizazi iliyopewa jina “Programu ya Kuelimisha,kwa kushirikiana na (BVGH).
Kampeni ya mwezi mmoja ilianza Septemba 7, katika Wilaya ya Bugesera. Inalenga wanawake wenye umri wa makamo 51,000 kutoka miaka 30 hadi 49 na watu wanaoishi na VVU / UKIMWI wenye umri kati ya miaka 25 hadi 49.
“Huo ni mpango wa majaribio, sio tu katika Wilaya ya Bugesera lakini katika maeneo mengine ya nchi pia, tunatoa wito kwa wanawake wote wanaostahiki kuja kwa uchunguzi na kupata matibabu mapema wanapogunduliwa,” alisema Dk Marc Hagenimana, Mkurugenzi wa Kitengo cha Magonjwa ya Saratani huko RBC.
Kati ya visa 5,000 vya saratani ambavyo viligunduliwa nchini Rwanda mwaka jana alisema, saratani ya kizazi ilikuwa ya pili kuenea zaidi baada ya saratani ya matiti.
Saratani ya kizazi imeongezeka zaidi ya mara mbili nchini Rwanda kwa miaka minne iliyopita, ikiongezeka kutoka visa 2,115 mnamo 2015 hadi 5,040 mnamo 2019,Kesi hizo zilipanda hadi 750 2020.