BERLIN, UJERUMANI

SHIRIKA la Afya Duniani WHO leo limefungua kituo cha kutoa tahadhari za mapema kuhusiana na majanga mjini Berlin kwa lengo la kujumuisha utaalamu na vifaa kwa ajili ya kukabiliana na majanga katika siku zijazo.

Kuelekea kufunguliwa kwa kituo hicho, shirika hilo la afya limesema kituo hicho kitawaleta pamoja washirika kutoka kote duniani watakaoshirikiana kubuni vifaa na data zinazohitajika kwa nchi zote kujiandaa, kugundua na kukabiliana na hatari ya majanga.

Kituo hicho kitazinduliwa na mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Kufuatia hatari iliyosababishwa na janga la Covid-19 wataalam wa afya wanaamini haitochukua muda kabla janga jengine halijaikumba dunia.