LONDON, England
KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amethibitisha klabu hiyo kuanza kufanya mazoezi na kiungo wake wa zamani, Jack Wilshere.

Wilshere anarejea Arsenal kama mchezaji huru baada ya kuachana na Bournemouth. Japokuwa, kurejea kwa Jack haimaanishi klabu hiyo itamsajili na badala yake amepewa nafasi ya kuendelea kujiweka imara akiwa na washika bunduki hao kwenye mazoezi ya timu hiyo.

Arteta amenukuliwa akisema:”Tupo tayari kumsaidia (Jack) kwa chochote ambacho tunakiweza. Analijua hilo na hiyo ndiyo hali halisi”,(Goal).