NA MWANDISHI WETU

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi jna  Septemba 20 kimewasili salama katika ardhi ya Tanzania kikitokea nchini Nigeria.

Mabingwa hao mara 27 wa ligi kuu Tanzania Bara walikuwa wakipambana kwa ajili ya kupeperusha bendera kimataifa kwenye ligi ya mabingwa Afrika.

Deni lao kubwa ilikuwa ni kwenye kupindua meza kibabe mbele ya Rivers United kwa sababu katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa Yanga ilifungwa bao 1-0 hivyo walitakiwa kushinda mabao zaidi ya mawili.

Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Rivers United mchezo ulipokamilika walianza safari kurudi Tanzania.

Yanga walitumia ndege ya Shirika la ndege la Tanzania na wamewasili salama nchini.