Mipango ni kuvua bahari kuu

Matunda yaanza kupatikana

NA ZAHOR SULEIMAN, ZAFICO

KATIKA kuleta maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imeifufua upya kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO)ambapo juhudi kadhaa zimechukuliwa ili kuona kampuni hiyo inafanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Pamoja na mambo mengine Kampuni ya uvuvi Zanzibar (ZAFICO) pia imesha watafutia masoko ya uhakika ya ndani na nje wavuvi nchini ili kuondokana na ugumu wa kimaisha.

Akizungumza na Makala haya, Dk. Ameir Haidar Mshenga, ambae ni Mkurugenzi Muendeshaji wa kampuni ya ZAFICO, alisema kuwa zoezi la kuvua bahari kuuu limeshaanza na kwamba wanatarajia kuweko kwa mabadiliko makubwa ya kampuni pamoja na watendaji na wavuvi kwa ujumla.

“Tayari tumeshaanza kuvua bahari kuu kwa kutumia vifaa na mitego ya kisasa baada ya ule wa awali kuwa na changamoto nyingi”, alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema kwa kuwa vifaa vyote vipo ikiwa ni pamoja na boti za uvuvi na vitendea kazi vyengine ni wazi kuwa kampuni hiyo sasa itaingia katika ushindani wa kazi ya uvuvi.

Aidha alifahamisha kuwa Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, wakati alipofanya kampeni zake za urais 2020 hakuacha kutamka uvuvi wa bahari kuu kila anapo pita hivyo alisema Serikali imetekeleza kwa vitendo ahadi hiyo ambayo kwa sasa ipo tayari kwa utekelezaji.

“Kwa asilimia kubwa ajira zimetegemea zaidi sekta ya uchumi wa bluu, sekta ambayo ni ukweli usiopingika bado hatujaitumia ipasavyo.”, alisema.

Mkurugenzi huyo, alisema kwa kuzingatia ahadi za mheshimiwa Rais katika kampeni na pamoja na ilani ya CCM kuhusu ajira 300,000 ZAFICO wameweza kubuni miradi mbalimbali ili kuhakikisha inakidhi ahadi ya Rais.

Aidha, ZAFICO pia inakusudia kununua dagaa kavu kwa wajasiriamali baada ya kupewa mafunzo ya njia za kisasa za uanikaji ili kuona linakuwa la kiwango bora.

“Tutawapa mafunzo wajasiriamali wa dagaa kavu na kuanikwa kwa kutumia njia za kisasa ili kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa pamoja na kufanya mafunzo ya vitendo kwa waanika madagaa kwa kutumia tekonologia hiyo, na kuliuza nje ya nchi”.

Aidha alisema ZAFICO itaanza kutoa rlimu kwa wavuvi ndani ya kipindi hiki kifupi hatua kwa hatua ili kuanza nao kuvua bahari kuu ambapo boti 1,000 zilizo ahidiwa na Serikali zitakapo kuwa tayari elimu hiyo iwe imesha wafikia walengwa.

Vile vile katika kuliinua dagaa la Zanzibar kitaifa na kimataifa, Mkurugenzi huyo alisema ZAFICO imekusudia kuanza na wajasiriamali waanikaji wa dagaa wa Shehia za Kama, Bububu na Kihinani, Ngalawa Wilaya ya Magharibi ‘A’.

Alisema ili zoezi hilo lifanikiwe, Serikali imetenga eneo maalumu la Kama ili kutumika kwa kazi hiyo ambapo wajasirimali hao tayari wameshaarifiwa na kwa kinachosubiriwa ni kukamilika kwa utengenezaji wa chanja.

Mkurugenzi Mshenga alisema tenda ya utengenezaji wa chanja hiyo imepewa Chuo cha sayansi ya Ufundi na Teknolojia cha Karume na kwamba iko katika hatuua ya mwisho ya nutengenezaji.

“Tunategemea mwezi ujao tutakuwa tayari utengenezaji wa chanja umeshakamilika kwa chanja 50 kwa kuanzia hivyo wajasiriamali wakae mkao wa kula kuchangamkia kazi hiyo”, alisema.

Awali Rais Dk Hussein Mwinyi, aliwahi kunukuliwa akisema muda wa kupoteza haupo hivyo alitaka ahadi zake kwa wananchi zitekelezwe kama alivyo waahidi ikiwemo kuipaisha Zanzibar kiuchumi kupitia Bahari Kuu ambapo ZAFICO inatekeleza kwa vitendo ikiwemo kutoa hizo nyezo za kisasa za uanikaji dagaa hali itatajiwa kuibua ajira zaidi 2,200.

“Boti ya Sehewa 02 ilitarajia kwenda kuvua bahari kuu ikiwa na vifaa vya kisasa na wataalamu walio bobea na inatarajiwa kurudi na tani nyingi za Samaki, tunatarajia kupata.

Kwa upande mwengine Mkurugenzi huyo alisema wanatarajia kulikarabati jingo la ofisi na utunzaji samaki lililoko Malindi kutoka kwa wataalamu wa chuo cha Sayansi ya Ufundi Karume.

Akizungumza na makala hii Ali Makame Kifundi mjasiriamali wa uanikaji Dagaa Ngalawa Kihinanai ammesema kuwa hapa tulipo tnafanya kazi hii kimazowea tu wakati mwngine hasara tupu anakupimia anavyotaka na ananunua kwa bei anayoitaka nakwamia limekosa viwango ambapo wanunuzi wetu wengi kutoka Bara na Congo.

Sasa Serikali kama imeliona hili la kutupatia bei muafaka na kuanika dagaa letu kwa kutumia tekonilogia rahisi ni vyema tunawaomba hao ZAFICO waharakishe kwani jambo hili tumelisikia tokea mwezi uliopita kua linakuja tunaomba lifike kama sasa Alisema Bw. Kifundi.

Hassan Khamis mwanakijiji wa Kama ambae ni mjasiriiamali wa kuanika dagaa wa Kama yeye amelezea kuufurahia amuzi wa serikali kwani eneo wanalo lianikia Dagaa ni la Mtu biinafsi na wanalipa kodi ya 15,000 kwa mwezi na kinguilio cha Sh 120,000 sasa  faida hapo tunagawana wakitupatia hayo maeneo na hizo nyezo bure ni ukpombozi  mkubwa na watakuwa wanafanya kwa weledi kazi walio pewa na Rais ya uchumi wa buluu