KIGALI, RWANDA
BODI ya TVET ya Rwanda (RTB) imetia saini makubaliano ya Rwf5.7 bilioni na Jumuiya ya Ulaya (EU) ili kutoa nguvu kazi yenye sifa katika sekta ya utalii nchini.
Hiyo itafanywa chini ya mradi uliopewa jina la Ubukerarugendo Imbere iliyozinduliwa Septemba 29 na inatarajiwa kuanza kwa miaka minne.
Mkurugenzi Mkuu wa RTB, Paul Mukunzi alisema kuwa Mafunzo ya Ufundi (TVET) ndio njia bora zaidi katika kuunda kazi za kupambana na umasikini katika jamii za Rwanda wakitaka juhudi za pamoja kufanikisha lengo hilo.
Alisema kuwa mradi huu unazinduliwa kwa wakati unaofaa, kwani TVET inaendelea kuboreshwa kwa ubora wa utoaji wa mafunzo na kuongeza msaada kwa sekta binafsi.
Alifafanua kuwa nchi inakuwa kivutio cha utalii na kitovu cha mikutano ya kimataifa na shughuli tofauti ambazo zinahitaji nguvu kazi.
“Sekta za utalii na ukarimu zina nafasi kubwa za biashara na tunahitaji kuwa tayari kuboresha utoaji wetu wa huduma na mteja ili kuongeza faida,”alisema.
Walengwa wa mradi huo mpya ni pamoja na wanafunzi, wakufunzi, mameneja wa skuli, skuli za umma na za kibinafsi za TVET zinazohusika katika sekta ya utalii na ukarimu.
“Tutafanya kazi kwa karibu na Rwanda Polytechnic (RP) pamoja na sekta binafsi, waongoza watalii, hoteli, mikahawa na mfumo mzima wa mazingira wa TVET nchini Rwanda,” alisema.