TUMEZOEA kula vya kula vya aina mbalimbali ambapo sehemu zote duniani zina aina za vyakula vilivyoeleka kuliwa. Chakula na mapishi kwa ujumla huchukuliwa kama sehemu ya utamaduni.

Hata katika sehemu moja ya jamii na kwenye familia mtu mmoja anapenda chakula cha aina fulani lakini mwengine asikipende chakula hicho sio kwa kuchukizwa kwa ladha yake na harufu, bali akikitia mdomoni humdhuru.

Wakati mwengine watu wawili mnaweza kula chakula cha aina moja, lakini mwengine atakuwa sawa kiafya mwengine kitamdhuru sana kiasi cha kudhoofisha afya yake.

Kuna baadhi ya aina za vyakula vinapochanganywa hugeuka kuwa sumu ya kumdhuru mlaji na hata kusababisha kupoteza maisha. Vifuatavyo ni aina za vyakula endapo vitachanganywa vinaweza kuwa sumu inayoweza kumdhuru mlaji.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa lishe kutoka nchini Nigeria, Habiba Haruna aliwahi kunukuliwa akisema kuwa zipo aina sita za chakula ambazo zinaweza kuwa sumu kwa mtu yeyote, endapo vitachanganywa.

Samaki na Maziwa, ni vyakula vyenye virutubisho muhimu kwa maisha ya mwanadamu lakini kuvichanganya sehemu moja vinaweza visiwe na uwezo wa kutengeneza virutubisho sahihi, hali hiyo inaweza kuleta shida baadaye.

Mwili wa binadamu hauhitaji vyakula vya aina tofauti vyenye kemikali za aina moja kuchanganywa na kufanya hivyo kunaweza kusababisha sumu itakayopelekea mtu kutapika na hata kuharisha.

Maji ya limao na Maziwa, huwa haviwezi kukaa sehemu moja kwani vikichanganywa lazima maziwa yaweze kukatika. Ikiwa mtu atachanganya maziwa na maji ya limao anaweza kutengenezea sumu, vilevile yanaweza kuleta shida katika moyo.

Karanga na Mafuta ya mzeituni, karanga ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binadamu na hutumika katika sehemu nyingi sana.

Pia karanga ina kiwango kikubwa sana cha protini na wanga, vilevile karanga ni moja ya virutubisho muhimu katika lishe, haswa kwa wale ambao wanataka kupunguza uzito.

Kwa mafuta ya mzeituni yanamsaada mkubwa pia hasa katika masuala ya tiba kwa baadhi ya magonjwa, lakini mchanganyiko wa mafuta hayo na karanga yanaleta shida ila inashauriwa kutumika pale moja inapokosekana lakini sio kwa pamoja.