NA SAIDA ISSA, DODOMA

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameongoza viongozi wakitaifa na watanzania katika zoezi la kumuuga mwili wa aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, William Tate Ole Nasha ambaye pia alikuwa mbunge wa jimbo la Ngorogoro mkoani Arusha.

Marehemu Ole Nasha alikutwa na mauti usiku wa kuamka juzi nyumbani kwake maeneo ya Medeli, jijini Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Rais, Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango alisema marehemu alikua na mchango mkubwa bungeni akitolea mfano namna ambavyo tetea mswada wa sheria wa fedha nakusema kuwa marehemu alikua mzalendo kwakuipenda nchi yake na mchapakazi hivyo kuna mengi yakujifunza kupitia maisha yake.

“Kuna mengi yakujifunza kwa marehemu kwani alikuwa mchapakasi hasa katika masuala ya kujenga nchi alihakikisha anajenga hoja mfano katika mswada wa sheria wa fedha marehemu alisimama nakujenga hoja zenye mashiko”, alisema Makamu wa Rais.

Kwa upande wake, waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizungumza namna ambavyo marehemu alifanya kazi kubwa ya kuhakikisha uwekezaji nchini unakua kwa lengo la kuimarisha uchumi wa nchi.

“Serikali imempotoza mtu makini sana nawaomba familia muwe watulivu katika kipindi hiki kigumu kwani sote tunajua wakati mnao upitia kwa sasa”, alisema waziri Mkuu.

Naye Spika wa Bunge, Job Ndugai akieleza namna walivyofanyakazi pamoja kipindi cha uhai wake.

“Katika kipindi cha uhai wake marehemu alikuwa ni mtu wa kuonesha mifano yakuigwa hasa katika maslahi ya wananchi hakika tumeondokewa na mtu muhimu sana”, alisema Ndugai.