PARIS, UFARANSA
MAHAKAMA moja nchini Ufaransa imemkuta rais wa zamani wa nchi hiyo Nicolas Sarkozy na hatia ya kufadhili kampeni kinyume cha sheria.
Alihukumiwa mwaka mmoja gerezani lakini ataruhusiwa kutumikia kifungo hicho nyumbani kwa kuvaa bangili ya elektroniki ili kufuatiliwa.
Sarkozy aliandamwa na mfululizo wa makosa ya kisheria.
Alishtakiwa mwezi Machi kwa kujaribu kumhonga jaji miongoni mwa mashitaka mengine.
Amekuwa rais wa zamani wa kwanza katika historia ya hivi karibuni ya Ufaransa kuhukumiwa kifungo.
Sarkozy aliiongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 2007 hadi 2012 na bado ana ushawishi mkubwa miongoni mwa wahafidhina wa Ufaransa.
Mwanasheria wake alisema atakata rufaa.