NA VICTORIA GODFREY

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea leo kwa michezo miwili kupigwa kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Simba itashuka dimbani dhidi ya Dodoma Jiji mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Simba inashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Biashara UTD, katika mchezo uliochezwa Septemba 28 kwenye Uwanja wa Karume ,mkoani Mara.

Dodoma Mji wanashuka dimbani wakiwa na furaha ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mchezo uliochezwa Septemba 28 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mchezo mwingine utakuwa kati ya Biashara watavaana dhidi ya Ruvu Shooting mchezo utakaochezwa Uwanja wa Karume Mara.

Ruvu Shooting itarusha karate yake  wakiwa na machungu ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao Dodoma Mji,hivyo watakuwa na kibarua cha kusaka pointi katika mchezo huo.