NA HAJI NASSOR, PEMBA
UONGOZI wa Umoja wa akinama wa CCM Tanzania ‘UWT’ wilaya ya Mkoani Pemba, umesema umeridhishwa na kazi ya utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025, inayofanywa na Mwakilishi wa Jimbo la Chambani.
Akizungumza hivi karibuni, Diwani wa viti maalum UWT wilaya yani humo, Hassina Sharif Mohamed, alisema kazi kutekeleza ahadi inayofanywa Mwakilishi huyo, wanaridhishwa nayo.
Diwani huyo alieleza kuwa, yapo mambo kadhaa yakiwemo aliyoshirikiana na Mbunge, madiwani na mengine aliyatekeleza bila ya kusubiri fedha za mfuko wa jimbo.
Alifahamisha kuwa, Mwakilishi huyo amekuwa akiendelea kuhakikisha wananchi wa Jimbo la Chambani wanaondokana na changamoto kadhaa.
“Sisi UWT Wilaya ya Mkoani, tunakushukuru na tunakupongeza kwa kazi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, na hivi ndivyo ambavyo tunawataka na wengine kuiga mfano wako,’’alieleza.
Hatua nyingine, Diwani huyo, alisema kilichobakia kwa sasa ni kuhakikisha wananchi kuweka kando tofauti zao, na kushirikiana na viongozi wao wa wadi na jimbo la Chambani ili kutekeleza vyema.