NA ABOUD MAHMOUD
HAMU ya mashabiki wa soka Zanzibar kushuhudia dabi ya Simba na Yanga katika fainali ya kombe la Mapinduzi imeyeyuka jana.
Dabi hiyo haitachezwa tena baada ya timu ya Yanga kutolewa hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo na Azam, kwa kufungwa mabao 9-8 kwa mikwaju ya penalti.
Mtanange huo wa nusu fainali ulipigwa kwenye dimba la Amaan majira ya saa 10:15 jioni na kuhudhuriwa na mashabiki wengi, wakiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman ambapo mchezo huo ulikuwa wa vuta nikuvute.
Timu hizo zilifanya mashambulizi huku kila mmoja akitamani kuingia fainali.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyopata bao.