NAIROBI, KENYA

KINARA wa Wiper Kalonzo Musyoka anatarajiwa kutangaza hatima yake kisiasa kufuatia kuvunjika kwa muungano wa OKA.

Kalonzo Musyoka na Gideon Moi wa KANU wamekuwa wa pekee waliosalia miongoni mwa vinara wanne wa OKA.

Tayari baadhi ya viongozi wa KANU wametoa taarifa wakikashifu hatua ya Musalia Mudavadi kujiondoa katika OKA na kuanza ushirikiano na Naibu wa Rais William Ruto.