KWA kipindi cha muda mrefu sasa nchi nyingi za Bara la Afrika zimekuwa zikiathirika katika suala zima la ukuaji wa kiuchumi pamoja na demokrasi bora kutoka na mapinduzi ya kijeshi yanayotokea mara kwa mara.

Ukiachilia mbali mapinduzi ya kijeshi yaliotoke nchini Sudan mnamo Oktoba 25 mwaka jana, wachambuzi wanatueleza kuwa tukio la kuondolewa madarakani kwa Rais Roch Kaboré ni mapinduzi ya nne Afrika Magharibi ndani ya miezi 17 iliyopita.

Itakumbukwa ya kuwa nchi jirani ya Mali imeshuhudia mapinduzi ya kijeshi mara mbili katika kipindi hicho, yakichochewa na wasiwasi juu ya kutoweza kukabiliana na kuongezeka kwa ghasia za wanamgambo wa Kiislamu.

Kwaupande wa tukio la Mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso ni jambo ambalo linaelezwa wazi kuwa sio tukio lilopokelewa vyema licha ya ukweli kuwa tukio hilo lilitarajiwa kutokea nchini humo.

Suala kubwa tunalojiuliza hivi sasa ni Je, vurugu za wanamgambo zilieneaje hadi Burkina Faso?

Tunaelezwa kuwa licha ya hali tete ya kiusalama na kisiasa ya Afrika Magharibi, Burkina Faso ilifurahia utulivu hadi uasi wa watu ulipomuondoa madarakani aliyekuwa Rais wa muda mrefu Blaise Compaoré mwaka 2014.

Tutakumbuka ya kuwa jaribio la mapinduzi la mwaka 2015 lilisababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya jeshi. Kaboré alichaguliwa mara ya kwanza mwaka huo kwa ahadi ya kuunganisha nchi.

Hata hivyo, wanamgambo kutoka nchi jirani ya Mali ambapo waasi waliotaka kujitenga mwaka 2012 walitekwa nyara na wanajihadi walifanya shambulio katika mji mkuu wa Burkinabè huku Kaboré akijiandaa kuchukua usukani.

Makundi yenye silaha yalichukua fursa ya uwepo dhaifu wa usalama katika maeneo ya mipakani ya Burkina Faso ili kuendeleza mashambulizi zaidi na kuimarisha uwepo wao.

Wanajihadi pia wamezusha mvutano wa kimadhehebu kati ya jumuiya za Kikristo na Kiislamu zilizokuwepo nchini Burkina Faso.

Aidha wamechukua fursa ya uwepo mdogo wa serikali na ukosefu wa usaidizi wa kibinadamu, ambao umeacha jamii zikiwa hatarini na kuzidhibiti na kuwasajili vijana kuwa wapiganaji.

Huku ikielezwa kuwa kwa kiasi fulani kwamba kisiasa pia umedhoofishwa na uwepo wa wapiganaji.

Mnamo mwaka 2020, wapiga kura ambao walikuwa wamekimbia makazi yao katika maeneo ya kaskazini na mashariki hawakuweza kushiriki katika kura ya urais ambapo Kaboré alichaguliwa tena kwa 58% ya kura.

Na kupelekea shinikizo za wanamgambo kwa jamii zilizidisha kutoridhika kwa umma katika muhula wa pili wa rais.

Hali ya matukio ya mapinduzi ya Burkina Faso yanawiana na matukio nchini Mali kabla ya mapinduzi yake ya kijeshi mwezi Agosti 2020.

Msururu wa mahsambulio hatari dhidi ya wanajeshi na raia uliofuatiwa na maandamano ya yaliyochochewa na kuongezeka kwa ukosefu wa imani kwa serikali ya Mali chini ya aliyekuwa Rais wa wakati huo Ibrahim Boubacar Keïta.

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Burkina Faso, Eddie Komboigo, amejaribu kuchukua fursa ya kutoridhika kwa umma kuhusu ukosefu wa usalama ili kuongeza ushawishi wake, Lakini umma huo nchini Mali, uliunga mkono kwa mapana mapinduzi ya kijeshi.

Hufo kubwa iliotanda ni kuwa Burkina Faso huenda ikakosa utulivu zaidi kwa kusimamiwa na jeshi.

Lakini tukiachana na jeshi la taifa hilo ipo haja ya kujiuliza je, tishio la wanamgambo wa kijihadi ni kubwa kiasi gani?

Wapo wanaoeleza kuwa hii ni sawa na ilivyokua Mali, kitendo cha kuondolewa kwa Kabore kulichochewa na hali ya kutoridhika miongoni mwa vikosi vya usalama kwa madai ya kutoungwa mkono kikamilifu dhidi ya wanamgambo wanaohusishwa na al-Qaeda na kundi la Islamic State.

Imeripotiwa kuwa siku ya Jumapili kulitokezea machafuko, katika kambi kadhaa za kijeshi, kwenye mji mkuu, Ouagadougou, na miji ya kaskazini ya Kaya na Ouahigouya.

Machafuko hayo yalifuatia miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya serikali, ya kumtaka rais huyo ajiuzulu.

Inaelezwa kuwa mashambulizi ya wanamgambo yaliyoanza mwaka 2015 yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 na kuwalazimisha watu milioni 1.5 kuyahama makazi yao, kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.

Huku skuli zikiwa zimefungwa katika maeneo kadhaa ya nchi kutokana na hatari iliopo.

Aidha imani kwa umma katika usimamizi wa rais juu usalama kwa raia ilishuka sana baada ya shambulio katika kijiji cha kaskazini cha Solhan mnamo Juni 2021. Ambapo zaidi ya watu 100 waliuawa katika shambului hilo linalodaiwa kutekelezwa na wanamgambo waliofika na kuingia nchini humo kutoka Mali.

Mashambulio ya Solhan yalisababisha maandamano ya kupinga utawala nchini, kumlazimu Kaboré kufanya mabadiliko katika serikali na kujiteua kama waziri wa ulinzi.

Shambulio lingine katika kambi ya kijeshi ya Inata ya kaskazini mnamo Novemba 2021 lilizidisha hasira dhidi ya serikali.

Zaidi ya maafisa 50 wa vikosi vya usalama waliuawa. Ripoti ziliibua kuwa kambi hiyo ilituma ujumbe wa dharura kuomba mgao wa chakula na vifaa vya ziada wiki mbili kabla ya shambulio hilo.

Rais alivunja serikali yake na kumteua waziri mkuu mpya na waziri waulinzi kabla ya mazungumzoya maridhiano ya kitaifa na upande wa upinzani.

Kwamujibu wa historia nchi zote mbili zilikuwa makoloni ya Ufaransa na Ufaransa imeendelea kudumisha uhusiano thabiti wa kiuchumi na kiusalama muda mrefu baada ya uhuru.

Sawa na Mali, vikosi vya usalama vya Burkina Faso vinategemea msaada kutoka Ufaransa ambayo ilipeleka wafanyakazi 5,100 katika eneo hilo chini ya kile kilichoitwa Operesheni Barkhane.

Hii ilianza wakati Ufaransa ilipotuma wanajeshi kudhibiti wanamgambo wa kijihadi waliokuwa wakiandamana kuelekea mji mkuu wa Mali, Bamako mwaka 2013.

Lakini uungwaji mkono wa umma kwa ushiriki wa Ufaransa umepungua huku hali ya usalama ikizidi kuzorota.

Mnamo Desemba, wakaazi wa Kaya walizuia msafara wa jeshi la Ufaransa kupeleka vifaa kwa jeshi la Burkina Faso kwa madai ya kuwa vikosi vya Barkhane vinafanya kazi na wanamgambo wa Kijihadi.

Itakumbukwa kuwa Ufaransa imefurushwa katika eneo la Sahel, ambalo linajumuisha nchi zote mbili, katika mzozo wa kidiplomasia na Mali ambao ulisababisha kujiondoa kwa karibu nusu ya kikosi cha Barkhane.

Tatizo la ukosefu wa usalama linaweza kutumiwa na wanajihadi, huku kukiwa na wasi wasi kwamba kukosekana kwa utulivu wa kisiasa kunaweza kudhoofisha ushirikiano wa ulinzi chini ya kikosi cha G5 Sahel ambacho kinajumuisha askari kutoka Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger.

Wakati Mali inageukia Urusi ili kuziba pengo hili la usalama, washirika wake wa Sahel – ikiwa ni pamoja na Burkina Faso wakipinga wamepinga vikali hatua hii yenye utata.

Viongizi wa mataifa ya Magharibi mwa Afrika wamekuwa na hofu kubwa ya usalama wao kutokana na mapinduzi ya kijeshi ya mara kwa mara katika ukanda huo.

Rais wa nchi jirani ya Niger, Mohamed Bazoum, alianza kwa kusuasua madarakani mwaka 2021 kwa jaribio la mapinduzi dhidi ya msingi wa mashambulizi mabaya dhidi ya raia na jeshi.

Kukosekana kwa utulivu nchini Mali na Burkina Faso pia kunasababisha wasiwasi wa usalama nchini Ivory Coast, jirani yao wa kusini.

Na kuelezwa kuwa kumekuwa na mashambulizi ya wanajihadi, tangu Juni mwaka 2020 yakilenga vikosi vya usalama.