ISLAMABAD, PAKISTAN

POLISI na majambazi wawili waliojihami wameuawa huku wengine wanne wakiwemo polisi wawili wakijeruhiwa wakati wa kurushiana risasi kati ya polisi na wahalifu katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Islamabad juzi usiku.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi tukio hilo lilitokea wakati polisi wakiwa kwenye ukaguzi wa kawaida wa ambapo watu wawili waliokuwa wakiendesha pikipiki waliamriwa kusimama, lakini mmoja wa waendesha pikipiki hao alichomoa bastola na kuwafyatulia risasi polisi, vyanzo viliiambia Xinhua.

Kutokana na hali hiyo, polisi mmoja aliuawa huku wengine wawili wakijeruhiwa. Polisi walifyatua risasi na kuwaua wahalifu hao wawili papo hapo, vyanzo viliongeza.

Kufuatia tukio hilo, polisi na vikosi vya uokoaji vilifika eneo hilo na kuwahamisha majeruhi na kuwapeleka katika hospitali iliyo karibu na jiji hilo. Uchunguzi umeanzishwa kuhusu tukio hilo.