NA AMEIR KHALID

MIAKA 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo tunasherehekea, tukiwa na fahari kubwa ya kujivunia mafanikio mengi ambayo yamepatika ndani ya miaka hiyo.

Kila mmoja atakuwa shahidi ya haya, kwani miaka mingi imepita tangu Zanzibar kupata uhuru wake kutoka kwa ukoloni wa sultani, ambao kabla ya hapo mambo mengi hayakuwa rahisi kuyapata.

Mbali na maendeleo mengi ambayo yamepatikana kwenye sekta tofauti, pia katika michezo huwezi kuiacha mbali kwani nayo pia imepiga hatua kubwa na kumekuwa na mabadiliko mengi ambayo yamepatikana katika kipindi cha miaka 58 ya mapinduzi.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejidhatiti katika kuhakikisha inakuza na kuendeleza michezo tofauti, kwa kuimarisha miundombinu ya kujenga viwanja vya michezo mbali mbali.

Ujenzi wa viwanja vya Amaan kwa Unguja na Gombani, ukarabati mkubwa wa viwanja vya Mao Zedong na kuwa vya kisasa kwa kuwekwa nyasi bandia, umeleta mafanikio mengi na kusahaulika shida za kutumia viwanja vibovu.

Tunaadhimisha miaka 58 ya Mapinduzi huku tukitembea kifua mbele tukijivunia mafanikio makubwa, yanayoendelea kupatikana katika sekta ya sanaa, michezo na utamaduni.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilianzisha Baraza la Sanaa Sensa na Filamu Zanzibar kwa madhumuni ya kusimamia, kufufua, kuhifadhi na kuendeleza sanaa zote za asili na za sasa.

Hatua hiyo imeiweka Zanzibar katika njia sahihi kiutamaduni kwa faida ya watu wa Zanzibar. Katika kufikia lengo hilo, Serikali imekuwa ikiendeleza utamaduni wake kwa kutumia mbinu tofauti kwa njia ya Sanaa.

Habari zaidi nunua gazeti la zanzibar leo