Zanzibar yapata sheria mpya ya dawa za kulevya

Usimamizi mazingira wapewa muhimu wa kutosha

NA KHAMISUU ABDALLAH

MAPINDUZI matukufu ya Januari 12 mwaka 1964, yanatimiza miaka 58, kama ingekuwa mwanadamu ni umri wa utu uzima mwenye wajukuu, hata hivyo tukilinganisha na umri wa mapinduzi katika ujenzi wa nchi, safari ndio kwanza inaendelea.

Tunaeleza hayo kwa kulinganisha na nchi zilizopitia kwenye mapinduzi barani Ulaya ambapo baadhi yao zina zaidi ya umri wa miaka 200, lakini hadi kufikia hatua ya kuitwa mataifa yaliyoendelea zaidi ya karne moja imepita wakichapa kazi usiku na mchana.

Hapana shaka mapinduzi ya Zanzibar ambayo naweza kusema ni miongoni mwa tunu zetu adhimu tuliyoachiliwa kama urithi na waasisi wa nchi yetu, ndiyo yaliyomrejeshea mzanzibari mzalendo utu wake, heshima yake na hadhi yake hasa kwenye maamuzi muhimu ya uendeshaji wa nchi.

Katika kipindi cha miaka 58, bila shaka yapo mengi ya mafanikio ya kimaendeleo yaliyofikiwa kama italinganishwa na kabla ya mapinduzi, ndio tafsiri hali ya neno mapinduzi ni kuimarisha hali, ustawi na maendeleo ya wananchi.

Habari zaidi nunua gazeti la zanzibar leo