Yasimamia vyombo muhimu vya maamuzi

Yatekeleza miradi ya kuinua hali za wananchi

NA HAFSA GOLO

MAPINDUZI ya Zanzibar ya Januari 12 ya mwaka 1964 yanatimia miaka 58, huku wazanzibari wote kwa ujumla wao wakijivunia maendeleo makubwa yaliyofikiwa kwa kipindi hicho katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mapinduzi ya Januari 1964, ndiyo yanayowafanya wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba wajiite na wajivunie uzanzibari, kwa sababu tu ndiyo yaliyowapa utambulisho wao utakaodumu milele na daima.

Tunaposema mapinduzi yameleta mageuzi hilo hakuna anaweza kulipinga, kwani tunathubutu kusema kila mwananchi wa Zanzibar anayeishi visiwa hivi ni mtumiaji wa matunda ya mapinduzi ambayo yameenea kila kona.

Moja katika wizara yenye jukumu kubwa katika usimamizi wa ustawi na uratibu wa maisha ya wananchi wa Zanzibar, ni Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Sera na Uratibu wa Shughuli za Baraza la Wawakilishi.

Ofisi hiyo inajengwa na taasisi muhimu na nyeti sana zenye kutoa huduma za moja kwa moja kwa wananchi wa Zanzibar, ambapo hivi karibuni waziri wa ofisi hiyo Dk. Khalid Salum Mohammed alitoa taarifa refu inayoonesha mafanikio kadhaa.

Habari zaidi nunua gazeti la zanzibar leo