Ujenzi skuli za kisasa za ghoroga washika kasi

NA HANIFA SALIM, PEMBA

 MIAKA 58 si haba hata kidogo, ni umri wa mtu mzima kabisa ya kuwa na watoto wakubwa pamoja na wajukuu.

Hivi sasa wananchi wa Zanzibar wanatimiza miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar mara baada ya kupata uhuru tarehe 12 Januari mwaka 1964 baada ya kupinduliwa kwa serikali ya kisultani.

Makala hii inaelezea namna ya sekta ya elimu ilivyoimarika kisiwani Pemba ukilinganisha na kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kama inavyoeleweka kuwa elimu ni sekta muhimu katika nchi yoyote ile kwani bila ya elimu hakuna utaalamu wa aina yoyote ni wazi kuwa watu hujifunza na kupata watalamu wa aina tofauti ikiwa ni pamoja na madaktari, wahandisi, wanasheria, wanahabari na taalumua nyengine tofauti.

Kabla ya Mapinduzi, Wazanzibari walibaguliwa na kukoseshwa elimu ya ngazi zote, watawala walifanya haya kwa dhamira ya kuendelea madhila kwa wazawa ili kuwa na ujinga wa milele.

Wakoloni wa kisultani walikuwa na mfumo wa kimagharibi kwa lengo la kuwapata watu wachache waliowatumikia wakati huo.

Kwa hivyo, elimu ilitolewa kwa misingi ya kitabaka na makabila, ambapo wanyonge wengi wan chi hii wakati huo hawakupata elimu.

LENGO LA SERIKALI KATIKA KUKUZA SEKTA YA ELIMU

Rais Dk. Hussein Mwinyi, alisema Sekta ya Elimu, imeelekeza jumla ya shilingi bilioni 69.0, sawa na (USD bilioni 30) ya fedha za Mkopo wa IMF kwa ajili ya kuzifanyia kazi changamoto mbali mbali zilizopo katika sekta ya elimu na kuimarisha kiwango cha elimu inayotolewa hapa nchini 33.

Habari zaidi nunua gazeti la zanzibar leo