NA MARIA INVIOLATA, DAR ES SALAAM

HISTORIA ya mwanadamu inaambatana na aina nyingi sana za vyakula vitokanavyo na  mimea,  hata hivyo ni  aina chache zinazolimwa kwa ajili ya chakula  na  biashara kutegemea sera za nchi husika na mazingira.

Mazoea ya kulima aina fulani kwa baadhi ya mikoa nchini na sera zinazobadilika badilika   kumepelekea  kudumaa kwa maendeleo ya kilimo na mkulima nchini.

Kwa mujibu wa Mhadhiri Mwandamizi Dkt. Robert Katikiro wa Idara ya Uchumi wa Kilimo na Biashara ya Chuo Kikuu Dar es salaam ili kufahamu ni namna gani idara hiyo inavyowaelimisha Watanzania umuhimu wa  kustawisha mazao tofauti yaliyozoeleka na hata yale ambayo hayajazoeleka lakini yana umuhimu mkubwa kwa wakulima!

Dkt. Katikiro anasema sera na ahadi za wanasiasa zinadidimiza maendeleo ya mkulima kutokana na kubadilika sera za kilimo kila mara na kutokua na muendelezo na vipaumbele vinavorandana na mipango ya muda mrefu wa taifa.

Gazeti hili lilipouliza iwapo Sheria ya Makazi (RA: The Resettlement Administration), iliyotiwa saini na Rais Franklin Delano Roosevelt iliyoasisiwa  na wanazuoni  Ilisaidia familia 500,000  kuhamia kwenye maeneo  salama.

Muasisi wa  sheria hiyo akiwa ni mwanazuoni  wa uchumi na masuala ya kilimo katika Chuo Kikuu cha Columbia Prof. Rexforg Guy Tugwell  aliyemuandikia Roosevelt  barua yenye muongozo mzuri wakati wa kampeni na mmoja wa kundi la wasomi wa chuo kikuu hicho waliosaidia kuaandaa sera ya Maendeleo iliyoongoza wakati wa Delano Roosevelt anagombea Urais.