NA MADINA ISSA

WAZIRI wa Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora, Haroun Ali Suleiman, amesema skuli ya Sheria Zanzibar itasaidia kuokoa fedha zilizokuwa zikitumika kusomesha wanafunzi wa masomo ya sheria kwa vitendo.

Akizungumza katika uzinduzi wa masomo hayo iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utawala wa Umma (IPA) Tunguu, mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema hatua hiyo ni kubwa ambapo siku za nyuma mafunzo kama hayo yalikuwa yakifanyika na taasisi za sheria Tanzania bara na kugharimu fedha nyingi.

Aidha aliongeza kuwa kuanzishwa kwa skuli hiyo ni ushahidi wa maendeleo ya sekta ya sheria nchini na kwamba itaimarisha ujuzi wa wanasheria wapya na mawakili wakongwe katika kuhakikisha haki inatendeka.