Samujel Kalu
MENEJA wa Watford, Claudio Ranieri amethibitsha kwamba klabu hiyo ipo katika harakati za kumsaini winga wa Bordeaux na Nigeria, Samujel Kalu kwa dau la pauni milioni tatu na pia ina azma ya kumsajili beki wa Liverpool, Nathaniel Phillips (24). (Evening Standard).

Kylian Mbappe
REAL Madrid inakaribia kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Paris Saint Germain, Kylian Mbappe (23) na atajiunga kama mchezaji huru wakati kandarasi yake itakapokamilika. (ESPN).

Tanguy Ndombele
KLABU ya Paris St-Germain ipo katika mazungumzo ya kumsaini kiungo wa Ufaransa, Tanguy Ndombele (25), kwa mkopo . Ndiye mchezaji aliyenunuliwa kwa kitita kikubwa wakati akijiunga na klabu hiyo 2019 kwa dau la pauni milioni 53. (Goal).

Anthony Martial
KLABU ya Sevilla bado inataka kumsaini mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa, Anthony Martial (26), kwa mkopo licha ya ombi lao kukataliwa, inaweza pia kumtafuta mshambuliaji mwengine wa Ufaransa na Lyon, Moussa Dembele (25) kama mbadala wake. (Marca).

Jesse Lingard
MANCHESTER United itamruhusu winga wa England, Jesse Lingard (29), kuondoka mwezi huu, huku Newcastle ikiwa na hamu ya kumsaini. Hata hivyo, mashetani wekundu hao hawatamruhusu Lingard kujiunga na West Ham au Tottenham kwa kuwa hawataki kuimarisha wapinzani wao waliopo katika nafasi nne bora katika msimamo wa Ligi Kuu England. (Sky Sports).

Mitchel Bakker
NEWCASTLE United wamewasilisha ombi la dau la pauni milioni 14.5 kumnunua beki wa kushoto wa Bayer Leverkusen na Uholanzi, Mitchel Bakker (21). (Mail).