NA HAFSA GOLO

WAJASIRIAMALI nchini wameipongeza serikali kwa kuwajengea uwezo na kuwapatia mitaji, mbinu za kutangaza na kupata masoko ya bidhaa zao.

Wakizungumza na Zanzibarleo kwa nyakati na maeneo tofauti ya mkoa huo hivi karibuni, walisema juhudi zinazochukuliwa na taasisi mbali mbali za serikali kuwapatia elimu ya uzalishaji bidhaa bora na namna ya uendeshaji biashara zao, zimeleta mabadiliko kwenye utendaji wa kazi zao.

Mmoja ya wajasiriamali hao anajishughulisha na useremala, Nassour Mbarouk, wa Mahonda wilaya ya Kaskazini ‘B’, alisema yapo matumaini ya kupata mafanikio zaidi kutokana na mashirikiano wanayoyapata kutoka serikalini.