NA KIJA ELIAS, MOSHI

AKIMA mama wajawazito wametakiwa kuwahi kliniki mara wanapohisi wana ujauzito na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya, ili kuwakinga watoto wanaotarajia kujifungua.

Wito huo, umetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania mkoa wa Kilimanjaro (UWT) Zuhura Chikira, wakati wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM ambapo UWT Wilaya ya Moshi mjini walifanya usafi katika Zahanati ya Njoro, pamoja na kutoa vifaa mbali mbali vya usafi katika hospitali hiyo.

Chikira amewataka akina mama kuacha mila za zamani, ambapo mwanamke anapopata ujauzito anapewa dawa za kienyeji, na kuwahimiza wajitahidi kuwahi kwenye zahanati, vituo vya afya, ili waweze kupimwa na wawe salama ili kuepusha vifo vya akina mama na watoto.