KIGALI, RWANDA

SERIKALI imepeleka walimu wakuu 9,985 kwa skuli za msingi na sekondari kwa lengo la kurekebisha mapungufu yaliyopo katika wilaya zote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Leon Mugenzi, mkuu wa idara ya usimamizi na maendeleo ya walimu katika Bodi ya Elimu ya Msingi ya Rwanda (REB) alisema kuwa licha ya kutumwa bado kuna nafasi zilizo wazi.

“Katika kila wilaya tulipobaini mapungufu katika skuli zao, tumekuwa tukiajiri tangu mwaka jana na tumepanga walimu hawa kwa skuli zilizowaomba,” alisema.Usambazaji mwengine wa walimu 1,687 wa skuli za msingi  kwa sasa unaendelea katika skuli zao, kulingana na Mugenzi.