GITEGA,BURUNDI

WANAJESHI wa Burundi wameripotiwa kuingia katika ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Chifu wa eneo la Lemera, Edmond Simba Muhogo aliliambia shirika la habari la AFP kuwa, vikosi vya Burundi viliingia katika eneo hilo la mashariki mwa DRC wiki iliyopita.

Alisema makomandoo hao wa Burundi wapatao 380 wameingia nchini Kongo DR kupitia wilaya ya Lemera iliyoko katika eneo la Uvira mkoani Kivu Kusini, kwa shababa ya kukabiliana na waasi wa Kirundi.

Chifu huyo alisema wanajeshi wa Burundi kwa sasa wanakabiliana na kundi sugu la waasi wanaobeba silaha katika wilaya za Bijojo na Bibangwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Habari zaidi nunua gazeti la zanzibar leo la tarehe 07 Januari,2022