LONDON, England
KLABU ya Watford imemfukuza kocha wake, Claudio Ranieri, ndani ya miezi mitatu tokea apewe kibarua cha kuinoa ambapo awali alisainishwa na kupewa mkataba wa miaka miwili.

Watford ilimuajiri Ranieri mwezi Oktoba baada ya kutumikia miaka miwili nje ya England, huku kufungashiwa virago kwa Xisco Munoz, ndiyo uliokuwa mwanga mpya wa Mtaliano huyo mwenye miaka 70 kupata nafasi tena kwenye EPL.

Ranieri alifanikiwa kuiongoza Watford kwenye michezo 14 huku akiwa ameshinda michezo miwili tu mmoja ukiwa dhidi ya Everton kwenye dimba la Goodison Park huku mwengine dhidi ya Manchester United.