NA MWANDISHI WETU

WIZARA ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar imekubaliana na na benki ya NMB kutoa mafunzo kwa watembeza watalii ili kurasimisha shughuli zao waweze kukopesheka.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Fatma Mabrouk Khamis, alieleza hayo wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano kati ya wizara hiyo na benki ya NMB yaliyolenga kuinua shughuli za vijana wanaotembeza watalii nchini.

Alieleza kuwa kuna wapo mitaani bila vijana wengi wanaofanya kazi ya kuongoza watalii bila ya ujuzi na kuharibu taswira ya zanaibar hivyo makakati huo utawasaidia kuimarishawa ujuzi na maarifa yao.