NA HAFSA GOLO

SHIRIKA la umeme Zanzibar (ZECO) limewataka wananchi kuacha tabia ya kujenga karibu na miundo mbinu ya umeme ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza.

Akizungumza mara baada ya kufanya matengenezo kwa nguzo iliyoanguka huko Mwembemakumbi, Meneja Mwendeshaji wa shirika hilo, Haji Silima, alisema ujenzi holela katika miundombinu ya umeme kunasababisha shirika hilo kutofanya kazi zao ipasavyo yanapotokea matatizo katika maeneo hayo.

Alisema ni vyema wananchi kufuata sheria na taratibu zilizowekwa kwa kuzingatia mipango miji   wakati wanapofanya   ujenzi ili kurahisisha shirika kutoa huduma bora na kwa wakati.

“Iwapo wananchi watayaheshimu maeneo yaliyowekwa miundombinu ya umeme watatusaidia kupunguza athari ndani ya jamii sambamba na shirika kutumia fedha kupitia changamoto hiyo,” alieleza Meneja huyo.