NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa Mjini Mgharibi Idirisa Kitwana Mustafa amewataka waandishi wa habari nchini kushirikiana na jeshi la polisi katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kuona taaluma hiyo inaendelea kubakia salama.

Kitwana alisema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali na jeshi la Polisi yanayohusiana na usalama kwa waandishi wa habari na jeshi la polisi Mkoa wa mjini Maghribi, mafunzo ambayo yalifanyika katika ukumbi wa ZURA uliyopo Wilaya Mjini Unguja.

Alisema waandishi wa habari na jeshi la polisi ni vyombo vinavyo fanya kazi kwa pamoja hivyo ni vyema wakawa na mashirikiano ya karibu, ili kufanikisha utendaji wa majukumu yao.