NA LAYLAT KHALFAN

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Simai Mohamed Said, amekitaka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) na kampuni ya REMAX, kuhakikisha wanaunganisha nguvu zao kubuni jambo rasmi litakaloweza kusaidia madalali kuwapeleka katika mfumo rasmi unaokubalika duniani.

Aliyasema hayo katika mahfali madogo ya wahitimu wa kozi fupi inayohusiana masuala ya uongozaji na uwendeshaji wa masuala ya ardhi na mali zisizohamishika na kuwatunuku vyeti wahitimu 49, hafla iliyofanyika kampasi ya SUZA jijini Zanzibar.

Alisema kazi ya udalali ni biashara kubwa kwa kuwa kila siku watu wanauza na kununua ardhi, kukodisha huku wengine wakiwa wanaweka mikataba kwa lengo la kuunganisha nguvu zao kwa malengo yaliyofanana.