NA ASIA MWALIM

VIJANA nchini wameshauriwa  kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia  uchumi wa Buluu, ili kufaidika zaidi kuliko makundi mengine.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Msaidizi Idara ya Oganaizeshen na Siasa, James Chilwa, alipokua akizungumza na Muandishi wa habari hizi, Ofisini kwake Jimkana Mjini Zanzibar.

Alisema vijana wana mchango mkubwa wa kuleta maendeleo ya kiuchumi kutokana na uwezo walionao, wanapaswa kujituma ili kuongeza wigo wa kipato chao na pato la nchi.

Aidha alisema si jambo jema kuona fursa za ajira zinawafakia watu kutoka maeneo ya mbali, wakati wazaliwa ndio wanapaswa kunufaika zaidi.

Katibu Chilwa alisema, kupitia uchumi wa buluu vijana wana nafasi kubwa ya kupata ajira za muda na za kudumu pale wanapoamua kujiajiri ikiwemo kufanya shughuli za ukulima wa mwani, na majongoo.