NA ASYA HASSAN

SERIKALI Wilaya ya Kati Unguja, imesisitiza ushirikiano wa pamoja baina ya vyombo vya usalama na wananchi, ili kusaidia kudhibiti matukio ya uhalifu.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Marina Joel Thomas, alisema hayo alipokuwa akizungumza na maispekta wa shehia za Wilaya hiyo waliofika kujitambulisha hapo ofisini kwake Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Alisema mashirikiano ya pamoja baina ya maofisa hao na wananchi yatasaidia kurahisisha utendaji wao wa kazi pamoja na kupata urahisi wa kuwatambua wahalifu ili waweze kuwadhibiti.