NAIROBI, KENYA

SERIKALI ya Kenya imesema kuwa inatarajia uchumi wke kuimraika kwa asilimia sita mwaka huu baada ya kunawiri kwa asilimia tisa katika robo ya tatu ya mwaka wa kifedha wa 2021.

Serikali hiyo ya rais Kenyatta, baada ya kushuhudia ukuaji wa uchumi wake kupungua kwa asilimia 0.3 mwaka wa 2020/21 kutokana na athari ya maambukizi ya virusi vya Corona, pamoja na kiwango cha mfumko wa bei za bidhaa kupanda hadi asilimia 5.4 mwaka huo kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, ilisema kuwa kuongezeka kwa mapokeo ya fedha kutoka kwa raia wake wanaoishi ughaibuni kumesababisha uchumi wake kuimarika kwa asilimia 6% mwaka huu.

Haya yalibainika wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya kamati ya kitaifa ya utekelezaji wa maendeleo ya serikali, kupitia mawaziri mbalimbali na washirika wa maendeleo, mabalozi wa nchi za kigeni na wawekezaji nchini Kenya.