NA KHAMISUU ABDALLAH

MAHAKAMA ya Wilaya Mwanakwerekwe chini ya Hakimu Johari Ali Makame inatarajia kusikiliza ushahidi wa kesi inayomkabili mshitakiwa John Mikodem (22) mkaazi wa Mtendeni ifikapo Machi 24 mwaka huu.

Kusikilizwa kwa ushahidi kunatokana na mshitakiwa huyo kukataa kosa lake kupatikana na kiwango kidogo cha dawa za kulevya katika maeneo ya Ng’ambo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Mwendesha Mashitaka Wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Fatma Ali, aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo tayari umeshakamilika na kuomba kupangiwa tarehe nyengine kwa ajili ya kuwasilisha mashahidi.