ROMELU LUKAKU

PARIS ST-GERMAIN wanahusishwa katika mazungumzo ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku mwaka mmoja tu baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 28 kuwagharimu Blues pauni milioni 98 kutoka Inter Milan. (But via Sun)

ERIK TEN HAG

RB LEIPZIG wanajaribu kupata dau la meneja aliyeteuliwa na Manchester United Erik ten Hag kutoka Ajax kama meneja wao mpya . (Telegraph – subscription required)

DARWIN NUNEZ

MANCHESTER UNITED na Arsenal wamejiunga na mbio za kumshaka Darwin Nunez baada ya kutuma ujumbe wake kumfuatilia mshambuliaji wa Uruguay mwenye umri wa miaka 22 wikendi ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Benfica. (Mirror)

ERLING HAALAND

MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund Erling Haaland, 21,amepuuzilia mbali nia ya kujiunga na klabu ya Manchester United kwa sababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway haamini kuwa wanaweza kutimiza matamanio yake ya ndani ya uwanja. (ESPN)

JESSE LINGARD

ROMA, AC Milan na Juventus wamejiunga na West Ham pamoja na Newcastle katika kuelezea nia yao ya kusaini mshambuliaji wa Jesse Lingard, 29, wakati mkataba wake katika Manchester United utakapomalizika msimu huu. (Mirror)