MIAMI, Marekani
KAMA ambavyo LA Lakers walivyoshindwa kutetea ubingwa wa NBA msimu ulioisha, Milwaukee Bucks wamevuliwa rasmi ubingwa msimu huu.
Bucks walitwaa ubingwa wa NBA msimu ulioipita na wameendelea kufanya vizuri msimu huu ambao walikuwa wanautetea, lakini, mbio zao zilimalizika mbele ya Boston Celtics.
Celtics waliwashushia kipigo kikali Milwaukee kwa kuwafunga kwa pointi 109-81 na kuwatupa nje ya safari ya ubingwa msimu huu.
Licha ya Giannis Antentokounmpo kutupia pointi 23, hazikutosha kufua dafu mbele ya Jason Tatum na nyota wenzake wa Celtics ambao walipindua meza kwenye ngwe ya pili baada ya Bucks kuongoza kwa pointi 26-20.Kwa matokeo haya, Celtics watachuana na Miami Heats kwenye fainali ya NBA Eastern Conference.(AFP).