NA HAJI NASSOR

MAHAKAMA ya Mkoa Wete, imempeleka rumande mshitakiwa Is-haka Rashid Hadid, baada ya kupandishwa kizimbani akidaiwa kutenda makosa manne kwa mtoto mwenye miaka 16, likiwemo la kubaka.

Akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha mashtaka, Juma Mussa, alidai mshitakiwa huyo alimbaka mtoto huyo ambae yuko chini ya uangalizi wa wazazi wake.