PARIS, Ufaransa
MHAMASISHAJI wa mtandao wa ‘YouTube’, Logan Paul, amesema, anatarajia kumpeleka bondia, Floyd Mayweather, mahakamani kwa kushindwa kukamilisha malipo yake.

Logan na Floyd Mayweather walikutana ulingoni Juni mwaka 2021, ikiwa ni takribani mwaka mmoja sasa.

Nyota huyo wa mtandao wa YouTube, anadai, mpaka sasa hajalipwa ada zake zote, na anachoka kusubiri.

“Hapana, hajanilipa malipo yangu yote, kwa sababu anapungukiwa na milioni kadhaa. Hili tunalipeleka mahakamani. Tutaonana mahakamani. Hongera kwa kwenda jela, Floyd”, Logan akinukuliwa na ‘The Mirror’.

Logan anahisi Mayweather anamdharau kwa kuwa yeye ni chipukizi kwenye biashara ya ndondi na amekuwa akifanya utani wa kusisitiza kuwa bondia huyo hana fedha kama anavyotajwa a kupewa jina la ‘The Money’. (AFP).