NA ZAINAB ATUPAE
MICHUANO ya mpira wa wavu ya Ligi ya Muungano, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mwaka huu ambapo timu 14 zitashiriki.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa Chama cha Mpira wa Wavu Zanzibar, Burhan Ali Khamis, michuano hiyo itakuwa ikifanyika katika viwanja viwili vya Ziwani Polisi na Magereza.

Alisema timu ambazo zitakazoshiriki michuano hiyo saba zinatoka Tanzania Bara na saba za Zanzibar.Alizitaja timu za Tanzania Bara ni Jeshi Star, Chui na Chuo Kikuu cha Kampala (wanaume) na kwa wanawake ni Chui, Magereza,Jeshi Star na Chuo Kikuu cha Kampala.

Kwa upande wa Zanzibar, timu za wanaume ni nne ambazo ni Mafunzo, KVZ, JKU na Nyuki huku wanawake zikiwa ni Mafunzo,JKU na KVZ.Akizugumzia juu ya zawadi, alisema, zitakuwepo lakini, kwa sasa hawatazitaja.

“Hatuwezi kuzitaja mpaka mambo yaweze kukamilika, tutazitangaza rasmi”, alisema.Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Mpira wa Ufukweni, Ame Msim, amesema, maandalizi ya michuano hiyo yapo vizuri.
Aidha, aliomba serikali kuuangalia mchezo huo ili kuzidi kuonekana kama michezo mengine.