NA ZAINAB ATUPAE
KOCHA Msaidizi wa Kikosi cha KVZ, Hussein Ramadhan, amesema, wamewasimamisha wachezaji saba kutona na utovu wa nidhamu.
KVZ inashika nafasi pili kwenye Ligi Kuu ya Zanzibar baada ya juzi kuifunga Polisi 1-0 na kufikisha pointi 49 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili huko Amaan, kocha huyo, alisema wachezaji hao wataendelea kutumikia adhabu hiyo hadi ligi hiyo itakapomalizika msimu huu.

Alisema, wamelazimika kutoa adhabu hiyo kutokana na utovu wa nidhamu wa wachezaji hao ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.
“Imani yetu itakuwa fundisho kwa wachezaji wengine, wataendelea kukaa nje hadi msimu utakapomalizika”.

“Kusimamishwa kwao sio tatizo, kwani tuna kikosi kipana ambacho kinafanyakazi zaidi ya hao”.”Wachezaji hao wahawakucheza dhidi ya Polisi na tulipata ushindi”.Aidha, alisema, mbali na kuwasimamisha wachezaji hao, wanakabiliwa na majeruhi wawili watakaosekana katika mechi zilizobakia.