LAGOS, Nigeria
SHIRIKISHO la Soka la Nigeria (NFF), limefikia makubaliano na kocha wa zamani wa Porto na Sporting Lisbon, Jose Peseiro, kuchukua majukumu ya timu ya taifa hilo.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 62, amejiunga na Nigeria baada ya aliyekuwa kocha wake,Gernot Rohr, kujiuzulu mwezi Agosti na kisha kuondoshwa kwenye kufuzu Kombe la Duniani na Ghana.

Moja ya mtihani mgumu kwake kwa hivi sasa kuiwezesha Nigeria kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) ambapo watacheza na Sierra Leone mnamo Juni 9 kabla ya kumenyana na Mauritius siku nne baadaye michezo ya kundi ‘A’.Kocha huyo bado hajasaini mkataba na Nigeria, lakini, imeelezwa atafanya hivyo kabla ya Mei 28.(Goal).