PAUL POGBA

MANCHESTER CITY wana nia ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 29, kwa uhamisho huru. (Mail)

PEP GUARDIOLA

POGBA angependa kufanya kazi na meneja Pep Guardiola na City wako tayari kumpatia ofa mshindi huyo wa Kombe la Dunia mkataba wa miaka minne. (Guardian)

ANTONIO CONTE

MENEJA wa Brighton Graham Potter ndiye anayependelewa kuchukua nafasi ya Antonio Conte katika Tottenham. Brighton wangetaka fidia ya pauni milioni 10 kutoka kwa Spurs iwapo Conte ataondoka mwishoni mwa msimu. (Telegraph)

ERIK TEN HAG

MENEJA ajaye wa Manchester United Erik ten Hag anamtaka mshambuliaji Mreno Cristiano Ronaldo kubakia katika klabu hiyo . Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake katika Old Trafford. (Telegraph)

GLEISON BREMER

CHELSEA wanaangalia uwezekano wa uhamisho kwa ajili ya mlinzi Mbrazili Gleison Bremer, 25. (Football London)

REIMS HUGO EKITIKE

MANCHESTER UNITED pia wana nia ya kumchukua mshambuliaji Mfaransa wa klabu ya Reims Hugo Ekitike mwenye umri wa miaka 19. (Mail)