Ousmane Dembele
KLABU ya Bayern Munich ina nia ya kumchukua mshambuliaji wa Barcelona, Ousmane Dembele (25), huku mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ukikamilika mwezi ujao. (Sky Sports).
Robert Lewandowski
CHELSEA inaweza kuungana na Barcelona katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland, Robert Lewandowski (33). (Guardian).
Jose Mourinho
NEWCASTLE United inataka kumshawishi kocha wa Roma, Jose Mourinho, atue St. James Park msimu huu licha ya mafanikio ya hivi karibuni ya kocha wa sasa wa ‘Magpies’, Eddie Howe (Marca).
Erik ten Hag
KOCHA ajaye wa Manchester United, Erik ten Hag, amesema, alikuwa na chaguo la kufanya kazi katika klabu tofauti, yenye msingi bora, lakini, akachagua kuchukua kazi Old Trafford. (De Telegraaf).
Kylian Mbappe
REAL Madrid wamekubaliana mkataba wa miaka mitano na mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 atahamia klabu hiyo ya Hispania kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake na Paris St-Germain utakapokamilika msimu huu wa joto. (Marca).
Tanguy Ndombele
LYON haitarajii kumsajili kiungo wa Tottenham na Ufaransa, Tanguy Ndombele kwa mkataba wa kudumu, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akitarajiwa kurejea London Kaskazini baada ya muda wake wa mkopo nchini Ufaransa. (Football Insider).
Kalvin Phillips
KLABU ya Newcastle na Aston Villa zinaongoza mbio za kumnunua kiungo wa Leeds na England, Kalvin Phillips (26), msimu huu wa joto. (Football Insider).