Andre-Frank Zambo Anguissa
KIUNGO wa Fulham, Mcameroun Andre-Frank Zambo Anguissa (26), ataendelea kubakia Napoli msimu ujao baada ya kujiunga nao kwa ajili ya mkopo mrefu mwezi Agosti mwaka jana. (Football Italia).

Sadio ManePARIS St-Germain ipo tayari kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Msenegal Sadio Mane (30), huku kukiwa na ripoti kwamba amekwama katika mkataba wake mpya. Mkataba wa sasa wa Mane unakwisha Juni 2023. (Sport Bild).

Kalvin Phillips
KLABU ya Manchester City ina nia ya kusaini mkataba na kiungo wa Leeds na England, Kalvin Phillips (26), huku wakiangalia mtu wa kujaza nafasi ya kiungo wa kati, Mbrazil Fernandinho (37), ambaye anaondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya miaka tisa. (Mirror).

Lisandro Martinez
MENEJA mpya wa Manchester United, Erik ten Hag, amemuongeza kiungo wa Argentina, Lisandro Martinez (24), kwenye orodha ya wachezaji anaowataka katika msimu huu. Martinez aliisaidia timu ya Ten Hag ya Ajax kushinda ligi ya Uholanzi 2021-22. (Telegraph).

Sergej Milinkovic-Savic
KLABU ya Manchester United, pia wanamtaka kiungo wa Lazio, Mserbia Sergej Milinkovic-Savic (27), ambaye alifunga magoli 11 na kusaidia upatikanaji wa magoli 11 katika mechi 36 za ‘Serie A’. (Calciomercato).

Alessio Romagnoli
CHELSEA inataka kumsaini nahodha wa AC Milan, Alessio Romagnoli (27), msimu huu katika uhamisho wa bila ya malipo. (Mundo Deportivo).

Robert Sanchez
KLABU ya Leicester City ipo tayari kumnunua mlinda mlango wa Hispania ambaye kwa sasa anaichezea Brighton, Robert Sanchez (24), ambaye amethamanishwa pauni milioni 50, huku mlinda mlango wa Denmark, Kasper Schmeichel (35), akiwa tayari kwa mazungumzo kuhusu mkataba wake na Foxes. (Telegraph).