TIMU ya soka ya Dula Boys imeungana na Kundemba kucheza ligi kuu ya Zanzibar msimu ujao, baada ya juzi kushinda mchezo wake wa mwisho kwa mabao 3-0 dhidi ya New King.

Mchezo huo ambao uliwafikisha pointi 60 sawa na Kundemba ambao wapo nyuma kwa mchezo mmoja, ulichezwa uwanja wa Kitogani Mkoa wa Kusini Unguja na kuwa na ushindani kiasi.