MICHUANO ya soka ya elimu bila malipo katika Mkoa wa Mjini Unguja kundi ‘A’ yameanza rasmi ambapo  timu za skuli za sekondari Jang’ombe na Kisauni zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.

Skuli ya Jang’ombe walianza kucheka na nyavu za Kisauni baada ya mchezaji wake Abdilah Ali kupachika bao katika dakika ya 10 lilidumu hadi dakika ya 25 Hussein Abeid wa Kisauni kusawazisha .