VIONGOZI wa Nchi Saba Zilizostawi Zaidi Kiviwanda Duniani, G7 wameitaka Urusi kusitisha mashambulizi yake kwenye miundombinu ya kilimo na usafiri.
Viongozi hao walitaka pawe na upitishaji huru wa bidhaa kutoka bandari za Ukraine.
Na walisema wataiwekea Urusi vikwazo zaidi na nchi yoyote itakayounga mkono juhudi za kuiba au kuuza nje nafaka ya Ukraine.
Mataifa ya G7 yamekuwa yakiahidi kuiwekea Urusi shinikizo zaidi kwa kuminya fedha zake.
Viongozi hao tayari wametangaza kupiga marufuku dhahabu ya Urusi.