WAZIRI Mkuu wa Japani Kishida Fumio na Rais wa Marekani Joe Biden wamekubaliana juu ya mpango wa kuweka ukomo wa bei ya mafuta ya Urusi kama sehemu ya juhudi za kuongeza shinikizo kwa nchi hiyo.

Viongozi hao pia walikubaliana wakati wa mkutano mfupi, pembezoni mwa mkutano wa G7 nchini Ujerumani kwamba nchi zao zitaimarisha muungano wao na kufanya kazi pamoja kuelekea kuwa na eneo huru na la wazi la Indo-Pasifiki.

Pia walisisitiza kwamba Japani na Marekani zitashirikiana kwa karibu katika kuiwekea Urusi vikwazo na kutoa msaada kwa Ukraine.

Maofisa wanasema ukomo wa bei ya mafuta ya Urusi utajadiliwa katika mazungumzo ya ngazi ya kikazi kati ya nchi hizo.

Hatua hiyo inalenga kuzuia Urusi kutumia mapato ya mafuta kufadhili uvamizi wa Ukraine.